Thursday, 17 July 2014

SAMAKI WA KUPAKA

\
\

MAHITAJI   
    samaki 2 aina ya tilapia
nyanya ya kopo
kitunguu maji 1
tangawizi 1
kitunguu saum 1
mafuta ya uto robo
pilipili(scotch bonnet pepper)    
tui la nazi zito 2 vikombe vya chai
curry powder 1/2 kijiko cha chai
bizari nyembamba ya unga kijiko cha chai 1/2
chumvi
girigilani

JINSI YA KUTAYARISHA.
   Marinate samaki na chumvi ,limau,kitunguu saum,tangawizi  kwa muda wa masaa 6 au zaidi.Baada ya hapo wakaange au waeke katika oven mpaka waive ila usiwakaushe sana.Baada ya hapo saga  pamoja  nyanya ya kopo,kitunguu maji ,kitunguu saum na tangawizi ,kisha bandika huo mchanganyiko jikoni na upike mpaka ukauke maji kisha  tia mafuta ,bizari, curry powder,chumvi na pilipili upike dakika  5.
    Badaa ya hapo tia maji  kidogo 1/2 kikombe cha chai pamoja na tui la nazi liive na mchumzi ubakie kiasi,waweke samaki kwenye sufuria ya kuokea na kisha umwagie huo mchuzi juu ya hao samaki na uwaroekee kwa muda wa 20 dakika ukisha toa kwenye oven katakata girigilani na utie kwenye hao samaki na hapo watakuwa tayari kwa kuliwa na unaweza kuwala na wali au ugali na chapati.

     by fatuma kh. chichi

1 comment: