MAHITAJI
1 kilo mchele wa basmati mrefu au pishori
1 kilo ya nyama iwe ya kuku au ngombe au mbuzi,kata katika umbo dogo la kutosha kula kisha uchemshe na tangawizi na kitunguu saumu,unga wa bizari pilipili manga na chumvi ili kuweka ladha nzuri.ikisha iva itoe iweke pembeni na mchuzi wake uweke pembeni utautumia badaae.
1 kilo ya vitunguu kata slice ya mviringo
1 kilo ya nyanya nyekundu zilizoiva,osha vizuri kisha katakata saizi ndogo ndogo sana.
240gram ya mafuta ya kupikia
2 maggi chiken soup cubes
3 kijiko kidogo cha chai unga wa pilipili nyekundu.
1/2 kijiko kidogo cha chai cha unga wabizari
3 kijiko cha chai unga wa girigilani(coriander powder)
2 kijiko kidogo cha chakula mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu saumu vilivyosaga
50gram majani ya girigalani osha na ukate.
8-12 mbegu za hiliki
15 mbegu nzima ya pilipili manga
JINSI YA KUANDAA
Weka mafuta katika sufuria yako iliyo juu ya moto tayari,kisha kaanga nyama yako iliyokwisha chemsah mpaka iwe rangi ya kahawia,kisha itoe nyama hiyo na ichuje mafuta ili mafuta yanayo baki weka kitunguuna endelea kukaanga kwa dakika 7-10 kisha weka unga wa bizari,pilipili nyekundu,girigalini,hiliki na pilipili manga.
Changanya vizuri mpaka upate mchanganyiko mzuri mkavu,miminia humo majiuliyochuja baadaa ya kuchemshia ile nyama yako na kuiweka pembeni ipoe.kisha weka nyanya fresh ndani ya sufuria yako pika mpaka maji yakauke na mafuta yaanze kuonekana kwa juu ndani ya sufuria.
Kisha weka nyama yako ndani ya sufuria polepole halafu punguza moto acha ijipike kwa muda mpaka mchuzi wako na nyama vikamate ladha pia usisahau kuweka chumvi kulingana na ladha unayoipenda.chukua sufuria nyingine weka mafuta ya samli na vitunguu ilivyoslice kisha kaanga na majani ya girigani,majani ya mint funika kwa dakika 10 kisha weka mchele wako mkavu uliokwisha oshwa vizuri na uchanganye vizuri,ongeza vikombe 5 vya maji na chumvi kidogo.mchele ukishaanza kuchemka funika sufuria lako na punguza moto ,maji yakiisha kukauka kiasi weka mchanganyiko wa ile nyama yako nusu thu juu ya wali wa basmati acha wali uive kabisa itakuwa tayari kula na pakua chakula chako kikiwa cha moto.
by fatuma kh. chichi
No comments:
Post a Comment